Uhuru siku ya jumapili amesema afisi za serikali ,biashara na kampuni zinafaa kuzingatia kuwaruhusu baadhi ya wafanyikazi wake kufanyia kazi nyumbani isipokuwa wale wanaohitajika kwenda afisini . Hatua hiyo inadhamiria kuzuia usambaaji wa virusi hivyo kupitia pesa zinazopokezana kwa watu . Wakenya wamehimizwa pia kuepuka maeneo yaliyo na watu wengi na kupunguza mikutano kama vile hafla za makanisani ,harusi na maazishi.
‘Epuka maeneo ya duka za jumla ,maeneo ya burudani na kupunguzo mrundiko wa watu katika magari ya usafiri wa umma kadri ya uwezo wake’ rais amesema .
Serikali pia imepiga marufuku usafiri wa kuingia na kuondoka nchini nan i wakenya walio na paspoti pekee ndio watakaoruhisiwa kuingia nchini endapo watpatikana na virusi hivyo na kuwekwa katika wadi maalum kwa matibabu na uangalizi .