(Text message) Video ya kuogelea uchi mto Turkwell yake Omondi ilimfanya Bob ku-mind

eric-omondi-kenya-1024x1024
eric-omondi-kenya-1024x1024

Mapema mwaka jana tarehe 3 machi 2018 staa na mtaalam wa ucheshi nchini Eric Omondi alijipata katika hali tatanishi baada ya kanda akiogelea uchi na vijana wa umri mdogo mto Turkwell kuvuja. Eric baadaye aliweza kutokea kusema pole kwa video kama hiyo na kuonekana kuomba msamaha kwa mashabiki wake.

"Kama mcheshi wakati mwingine mtu hufanya makosa. Ila nasema watu wanisamehe."

"Sijutarajia kama itafika katika mitandao ya kijamii. Sio lengo langu kuwakosea watu."

Mawasiliano ya simu ya mwisho ya Uhuru na Bob Collymore (Yaliyomo)

 Kisichofahamika na wengi ni kuwa aliyekuwa mkurugenzi wa Safaricom Bob Collymore alimtumia ujumbe mcheshi huyu baada ya tukio hilo.

Katika mtandao wake wa insta, staa huyu amechapisha ujumbe huo:

https://www.instagram.com/p/BzZ-9VTAIco/

"Saa sita na dakika arobaini na sita mchana alinitumia ujumbe huu. Akanipigia simu na kuniambia nimuone asubuhi ya siku iliyofuata." Eric Omondi.