Thamani, sifa na upekee wa Gulfstream G280, ndege aliyosafiria Kipchoge

EGUrV3ZXkAAe3O9-compressed
EGUrV3ZXkAAe3O9-compressed
Jeti aina ya Gulfstream G280 yenye thamani ya bilioni 2.4 ilitua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Eldoret.

Bingwa wa Olimipiki na mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge alipewa hadhi ya upekee Jumatatu usiku aliposafiria ndege inayomilikiwa na bwenyenye billionea maarafu sana wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe.

Kipchoge ambaye anatazamiwa kuvunja rekodi yake ya mbio za masafa marefu kwa chini ya saa mbili maarufu kama INEOS 1:59 Challenge alipewa hadhi ya hali juu sana na bwanyenye Sir Ratchliffe ambaye anafadhili mbio hizo.

Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kenya (KAA) kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Eldoret jana usiku walipokea ndege ya Sir Jim's , ambayo iliendeshwa na marubani wawili kutoka makao yake ya Uingereza na kumsafirisha Kipchoge kwenda mji mkuu wa Austria.

Ni huko Vienna ambako Kipchoge, mwenye umri wa miaka 34, anatarajiwa kushirki katika mbio za masafa marefu chini ya saa mbili. maarufu kama "INEOS 1:59 Challenge" iliyothaminiwa na Sir Jim, mmiliki wa kampuni ya kemikali ya INEOS.

Ndege aina ya Ghubastream G280, nambari ya usajili M-INTY ilisajiliwa Uingereza mnamo Machi 4, 2016, na mara ya mwisho ilionekana katika visiwa vya Uingereza ambayo ni makao makuu ya Sir Ratcliffe.

Ndege hiyo inaaminika kuwa na dhamani ya bilioni 2.5.