Master of the Game: Mwanamme aliyeoa wanawake 12 bila mmoja wao kujua

pjimage
pjimage
Jina la  Pius  Odeke ni kama  la mfalme katika  kijiji chake huko  teso kusini   kwa sababu mzee huyo wa miaka 76 ,alifanya  mengi ambayo wengi hadi leo wana maswali ya jinsi alivyoweza kuwa na  wanawake 12  nyakati hizi bila kugunduliwa hadi mwenyewe alipoamua kupasua mbarika .

Wanaumehufurika kwake ili kupata mafunzo ya jinsi ya kuweza kukabiliana na changamoto za ndoa za mke zaidi ya mmoja .Odeke alikuwa akifanya kazi na shirika moja la serikali huko Mombasa kwa miaka zaidi ya 40 tangu ujana wake na pesa hazikuwa tatizo . Wakati  akifanya kazi , shughuli zake nyingi zilihusisha kusafiri katika  mataifa ya afrika mashariki kwani wakati alipoanza kazi kulikuwa na jumuiya ya afrika mashariki na usimamizi wa bandari ulifanywa kwa pamoja kati ya nchi za Kenya ,Uganda na Tanzania .

Katika piga kazi zake ,Odeke alijipata ana wanawake  wanne  nchini Tanzania ,watatu nchini  Uganda , na watano humu nchini . wote hawakujua kwamba alikua na familia nyingine kwa sababu ya kazi yake kila mmoja aliamunu kwamba wakati hakuwepo basi alikuwa akifanya kazi .kati ya wake zake hao kila mmoja alikuwa na mtoto isipokuwa mmoja  wahumu nchini . Alipostaafu mwaka wa 2010,aliwaleta pamoja wanawak hao  kwa mara ya kwanza pamoja nawatotowao na wengine walizimia walipogundua kwamba muda wote mzee Odeke alikuwa na familia nyingine sio moja au mbili bali 12!

Kwa sababu kifedha hakuna malumbano yaliyodumu kwani  wengi walikuwa na watoto wakubwa na hata wengine waliokuwa wameshaoa au kuolewa .Aliwataka watoto wake ambao walikuwa na  dhamira y kujenga nyumba zao katika boma lake huko teso kufanya hivyo na waliotaka kurejea Uganda au Tanzania na mama zao pia wafanye hivyo na hapo ndipo sifa zake kama ‘mzee wa kimataifa’ zilipoanza kwa sababu kando na  kwamba hakuwa amewajua wanawe wote vizuri ,kulikuwa na mgongamano wa lugha katika boma lile kwa sababu watoto wake kutoka Uganda walizungumza kiingereza na kiswhaili adimu ilhali wale kutoka Tazania walifahamu Kiswahili kuliko kiingereza .Mzee  alijua jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo na mwisho wa  siku bibi zake 8 walikubali kujengewa pale kwake na likawa boma kubwa kama makavazi ya EAC  hadi leo .