Timmy Tdat aitetea Vitamin U, tupewe fursa ya kufanya video chafu

Vitamin-U-Video-tIMMY
Vitamin-U-Video-tIMMY
Msanii mwenye utata Timmy Tdat amefunguka kilichojiri ili kufuta wimbo wake ya Vitamin U kwenye mtandao wa YouTube.

Mkwaju huu ulikuwa ushaanza kupata mashiko na nafasi kubwa YouTube kisha ghafla ukatolewa.

Wengi wa wafuasi wake walihoji kuwa audio ilikuwa nzuri sana ila staa akachafua kwenye video.

Timmy amesema kuwa alifuta wimbo huu ili kumsetiri Rosa Ree kutoka kwa ghadhabu ya BASATA.

 Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Timmy alisema kuwa kuna vipande vitahaririwa kabla video hiyo ipandishwe tena YouTube.

“Nilitoa video sababu ya Rosa Ree..." Alianza kusimulia.

Timmy amesema kuwa BASATA ya Tanzania ilimjia juu sana Rosa Ree,

"Side ya Tanzania ilikuwa noma. Monday Tuesday na Wdnesday alikuwa kwa kesi tofauti. On Monday alikuwa sijui kwa akina nani, on Tuesday alikuwa kwa board ya filamu, on Wednesday alikuwa kwa BASATA yenyewe so the more ilikuwa inaendelea kukaa hapo ndio the more inakaa nikama yeye ni kichwa ngumu..." Aliendelea Timmy.

Aidha, Timmy amesema kuwa marekebisho yatafanywa na ngoma iwe freshi tena,

"You see those guys hawawezi kuelewa kwamba haiko kwa channel yake, iko kwa channel yangu na hawawezi kuelewa kwamba si ngoma yake ni yangu nimemshirikisha. Vile ameshakuwa mhusika ni noma already. Mimi kitu ningeweza kufanya the best ni kupull kwanza video, vitu zitulie alafu nipige edit,” Timmy

Timmy ameongeza kuwa serikali kupitia mamlaka ya kutathmini ubora wa filamu isiwe na misimamo migumu kuhusu kazi za wasanii,

“Nikipewa fursa ya kufanya video kama hio. Mimi naona ntaifanya kwa sababu huko ndio mahali tunaenda. Tray Songz wanazifanya, akina pretty ugly wanazifanya. We need to take our industry to the next level.”  Timmy