Digital-Addicts-La-Liga-spy-app-logo

Timu tano za kuangazia msimu ujao ligi kuu Uhispania

Laliga Santander inatarajiwa kung’oa nang’a hii leo huku mechi ya kwanza ikiwa baina ya bingwa mtetezi Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao.

Kwa muda sasa klabu ya Barcelona imekuwa ikitawala ligi hio huku Lionel Messi akiwakosesha usingizi mabeki pamoja na walinda lango wa timu pinzani. Hata hivyo, Vilabu vingine vimekuwa na biashara za kufana sana na huenda vikaletea mabingwa hao wakati mgumu msimu huu.

Atletico Madrid

atletico.madrid

Ronaldo kuwania tuzo la mchezaji bora dhidi ya Messi na Van Dijk

Bingwa wa mwaka 2014, Atletico Madrid ilimsajili kinda wa miaka kumi na tisa, Joao Felix kutoka klabu ya Benfica na sasa kinda huyu anatarajiwa kuendeleza ukali wake nchini Uhispania.
Pamoja naye, klabu hio ya uhispania ilinunua wachezaji saba wapya huku Kocha wao Diego Simeone akisema kuwa anataka kubadilisha aina ya mchezo wake. Atletico huenda ikarejelea makali yake ya msimu wa 2013/2014 ilipotwaa taji la Laliga.

Real Madrid

real.madrid

Zinedine Zidane amemsajili kiungo mshambulizi wa Chelsea, Eden Hazard ili aweze kumsaidia kungangania taji la ligi kuu nchini Uhispania.

Hazard anatarajiwa kurudisha furaha mioyoni mwa wapenzi wa klabu ya Real Madrid msimu huu haswa baada ya kukosekanana mfungaji wa kutegemewa msimu uliopita.

Zidane amefanya sajili nne kufikia sasa na huenda akamsajili Neymar kabla dirisha la Uhamisho halijakamilika.

Villareal

villareal\

Mastaa waliovunja uhusiano wao na klabu zao kimabavu

Santiago Carzola amerejea na raundi hii anakiwasha kama moto. Msimu uliopita kiungo huyu alianza akiwa majeruhi ila baada ya kurejea mwezi Januari kiungo huyu alipika magoli sita huku akicheka na wavu mara nne.
Villareal huenda ikaletea uchangamfu mwingi msimu ujao baada ya kuonyesha makali mwishoni mwa msimu uliopita.

Barcelona

valencia-cf-v-fc-barcelona-la-liga

Mkurugezi mkuu wa Barcelona Josep Martina aliweka wazi matamanio ya kuona klabu yake ikimaliza msimu kama haijapoteza mchezo hata mmoja.

Barcelona imemsajili Antoinne Griezmann pamoja na Frankie De Jong kuongeza kwenye kikosi cha Barcelona. Msimu uliopita Barcelona ilipoteza michuano mitatu pekee na sasa wanaazimia kuimarisha rekodi hio. Je wataweza?

Sevilla

sevilla

Sevilla imemleta aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania, Julen Lopetegui na sasa anatarajiwa kuleta ushindani mkali msimu ikizingatiwa kwamba alifukuzwa kazi msimu uliopita na klabu ya Real Madrid.

Hata hivyo, Usajili wake Rony Lopez, Luuke De Jong pamoja na Olivier Torres inatarajiwa kuongeza ushindani kwenye ligi kuu Uhispania msimu ujao.

Soma Mengi Hapa

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments