Timu ya Kenya ya wanariadha kurejea leo baada ya kumaliza wa pili, Doha

wanariadha(1)
wanariadha(1)
Timu ya Kenya ya riadha inatarajiwa nchini leo saa nane mchana kutoka Doha, Qatar huku waziri wa michezo Amina Mohammed akiwalaki katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Kenya ilimaliza ya pili, nyuma ya Marekani katika michezo hiyo wakiwa na medali 11, sawia na mwaka wa 2017 jijini London ambako walimaliza wa pili nyuma ya Marekani na medali tano za dhahabu, mbili za fedha na nne za shaba.  Jamaica ilimaliza wa tatu huku Uchina na Ethiopia wakifunga orodha ya tano bora.

Bingwa wa mbio za mita elfu 5 duniani Hellen Obiri anadai kuwa huenda akaamua kushiriki mbio za mita elfu 10 hivi karibuni. Haya yanajiri baada ya kutetea taji lake mjini Doha, Qatar katika mbio za ubingwa duniani zilizokamilika jana. Mwanajeshi huyo pia amaedai atachukua likizo ya mwezi mmoja kabla ya kuanza matayarisho ya mbio za olimpiki.

Kocha wa Everton Marco Silva anadai kuwa hana wasiwasi wowote na wala hayuko chini ya shinikizo licha ya kupoteza mara nne kwa mpigo katika mechi za ligi ya EPL. The Toffees wanashikilia nafasi ya 18 na alama saba baada ya mechi nane, na watahitaji kujimudu ili kukwepa shoka la kushushwa daraja.

Kocha wa Manchester CityPep Gurdiola anadai hana wasiwasi wowote licha ya kunyukwa mbili bila na Wolves jana na kusalia alama nane nyuma ya Liverpool katika ligi ya Uingereza.  Guardiola anadai bado kuna mechi nyingi sana za kucheza na chochote chaweza fanyika huku wakiwania kutetea ubingwa wao.

Juventus iliiaza Inter Milan 2-1 katika mechi ya kukata na shoka kweye ligi ya Italia, na kupanda kileleni mwa ligi na alama 19. Mchezaji wa akiba Gonzalo Higuain alitia bao la ushindi kunako dakika ya 80, Lautaro Martínez kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti katika kipindi cha kwanza, huku Paulo Dybala kuwapa Juve uongozi mapema. Inter walipoteza kwa mara ya kwanza msimu huu na kuwacha Juventus pekee  na rekodi ya kutopotea katika ligi ya Italia msimu huu.

Luis Suarez, Lionel Messi, Ousman Dembele na Arturo Vidal walifungia Barcelona na kuisaidia kunyuka Sevilla 4-0 katika mechi ya La liga jana. Ushindi huo uliwapandisha mabingwa hao hadi nafasi ya pili na alama 16, mbili nyuma ya Real Madrid.

Hata hivo Barca walimaliza mechi hio na wachezaji 9 baada ya Ousmane Dembele na Ronald Araújo wakionyeshwa kadi nyekundu. Kwingineko Atletico Madrid walitoka sare tasa na Real Vala-dolid na kushuka hadi nafasi ya tatu.