Timu ya nguvu:Tazama picha za watu wanaofanya kipindi cha Jacque Maribe kuwa bora zaidi

Mwanahabari Jacque Maribe amerejea tena katika kazi yake huku akizindua kipindi chake cha siasa kinachofahamika kama 'The hot seat'.

Ni kipindi ambacho kitawanyamazisha wakosoaji wake baada ya kuhusika katika mauaji ya Monicah Kimani na wengi kuona kuwa hatorudi tena katika utangazaji.

Maribe ambaye amefanya kazi katika kampuni ya uhanahabari tofauti kama vile runinga ya K24, Kiss na Citizen aliamua kuchukua hatua ya imani na kuanzisha kipindi yake na hawa hapa baadhi ya wafanyakazi ambao wanamsaidia katika kazi yake;

George Oraro – anafanya kazi ya kamera

Sarah Mwangi -Ni mzalishaji wa kipindi hicho yaani producer

Sarah pia anajitambulisha kama mwanahabari, mzalishaji na hata mnenaji wa hadharani, pia amefanya kazi na mwanahabari Betty Kyallo katika kampuni ya mediamax.

Omarih K Hiram– Mwelekezaji wa kipindi hicho.

Huku Maribe akianzisha kipindi hicho alikuwa na haya ya kusema,

“Unahisi kama kila kitu kinaenda shwari na sambamba maishani mwako hadi pale utakuja kufahamu kuwa dunia imekupangia vingine

Umekuwa palepale imekuwa roller coaster ya mwendeshaji anayejaribu kuchukuwa yote ndani na hata kujaribu kutabasamu hata kama huwezi

Lakini badala ya kukata tamaa kwa yote unasimama tena na kuchukuliwa na pembe.” Jacque Alisema.

Hizi hapa baadhi ya picha zao;