Timu ya AS Roma yazindua ukurasa rasmi wa Kiswahili

as roma
as roma
Klabu ya ligi kuu nchini Italia, AS Roma imezindua ukurasa wake rasmi wa lugha ya Kiswahili hapo jana mjini Rome, Italia.

Baada ya kumpa mwanariadha Eliud Kipchoge kongole kwa lugha ya Kiswahili kwenye Ukurasa wao wa Twitter. Mnamo siku ya jumamosi, AS Roma iliombwa na mashabiki wake kutoka Afrika Mashariki kuzindua Ukurasa rasmi wa lugha ya Kiswahili.

Waitaliano hawa waliwaahidi mashabiki wake kuwa watatekeleza matakwa yao siku yajumapili. Ahadi ni deni na hapo jana klabu hiyo  iliandikisha historia kwa kuwa klabu ya kwanza kutoka bara ulaya kuzindua ukurasa wao rasmi kwa lugha ya Kiswahili.

https://twitter.com/ASRomaSwahili/status/1184506491354734593

Lugha ya Kiswahili ndiyo inayozungumzwa na watu wengi katika mataifa ya Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda pamoja na Burundi.

AS Roma, almaarufu Giallorossi ilianzishwa mwaka wa 1927 mjini Rome Italia. Klabu hii inashikilia nafasi ya tano kwenye ligi kuu nchini Italia na alama kumi na mbili baada ya mechi saba.

Kwenye historia yake, Roma imeshinda taji la ligi kuu nchini italia mara tatu pamoja na mataji tisa ya Coppa Italia.

Baada ya kuzindua ukurasa huu, Mashabiki humu Afrika mashariki walichukua nafasi hiyo kuwa karibisha waitaliano hawa wakiongozwa na klabu ya AFC Leopards.

https://twitter.com/AFCLeopards/status/1184545521391804416

Habari na: Albanus Kiswili (Twitter: @Albanus_10)