Watiu hao walipoteza fahamu baada ya kunywa sanitizer iliyochanganywa na soda na maji amesema mkuu wa polisi wa Siddharth Kaushal wa mji wa Kurichedu katika jimbo la Andhra Pradesh.
Walikimbizwa hospitalini lakini wakatangazwa kuaga dunia pindi tu walipofikishwa .
Kundi hilo lilimua kutumia saniser kama kileo baada ya maeeo yote ya kuuza pombe kufungwa kufuatia agizo la serikali ya watu kutotoka nje ili kukabiliana na janga la corona .
Mamia ya watu huaga dunia kila mwaka nchini india kwa kunywa pombe hatari yenye sumu ambayo huuzwa kwa bei ya chini .
Wagemaji wakati mwingi huweka methanol kupindukia katika pombe na hata mafuta jambo ambalo husabaisha vifo vya watu wanaoitumia pombe kama hiyo ili kuzidisha kileo ndani yake .