Toboa Siri: Bwanangu Huniita Jina La Mamangu, Sikujua Anampiga Kuni Pia

Mrembo mmoja aliwashangaza watangazaji Mbusii na Lion katika kitengo cha 'Toboa Siri' alipofichua kuwa mumewe amempachika mamake mimba.

Mwanadada huyo alikiri kuwa shida ilianza wakati mmoja mumewe alirudi nyumbani akiwa mlevi chakari na badala amuite jina lake alikuwa anamuita jina la mamake.

Hapo alianzisha uchunguzi na ndipo aligundua kuwa wawili hao wana uhusiano. Isitoshe amempachika mimba.

"Mimi nimeolewa na nina mtoto moja. Nimekaa kwa ndoa kwa miaka miwili sasa tulikuwa tunakaa vizuri na mume wangu na ilifika mahali akaanza kubadilika, mara hali kwa nyumba na nikimuongelesha anajibu na hasira." Alisimulia mwanadada huyo.

Siku moja kwenye harakati zake za ulevi alianza kuniita jina la mama yangu. Sasa nikashindwa nini inaendelea na aliendelea kuniita ivo siku kadhaa. Naishi na yeye lakini mamangu yuaishi kivyake kwani ni single mother.

Nikakuja nikachunguza nikapata wana uhusiano pamoja na hata sahii mamangu (mwenye umri wa miaka 40) ana mimba na nashuku ni yake. Niliangalia message zenye hutumiana na hata mamangu humuita sweetheart." Aliongeza akidai kuwa hajui kama mamake mzazi anajua uhusiano wao.

Skiza uhondo wote.

&feature=youtu.be