Mbusii Deh

Toboa siri: Nikishiriki ngono mawazo yangu huwa kwa mpenzi wa zamani

Jamaa mmoja aliwaacha watangazaji Mbusii na Lion, vinywa wazi hivi majuzi alipofichua kuwa yeye hubidi amefikiria kuhusu mwanadada mwingine ili ‘amalize kazi’.

Kulingana na huyo jamaa, mwanadada ambaye yeye humuwaza aliyekuwa mpenzi wake wa kitambo kabla ya kumtenga na kurudi shuleni.

Anasema kuwa anahisi kuwa ana shida na angependa kupewa usaidizi  kutoka kwa waskizaji wa Radio Jambo. Aliongeza kuwa kama hatosaidika basi wapenzi wake anaoshiriki nao ngono wajue ukweli wa mambo.

Soma usimulizi wake,

Nimeshiriki ngono na wasichana wengi lakini kuna msichana mmoja ambaye mimi hufikiria kila mara ili nimalize kazi.

Nataka kutobolea wana Jambo siri hii ili wanishauri na pia ili hao wasichana wajue kuwa nikiwa nao mimi humfikiria msichana huyo ili niridhike. Msichana huyu nilikuwa kwa uhusiano naye kwa miaka miwili na karibu tufunge ndoa.

Msichana huyo alienda shuleni na tangia aondoke hapo ndipo hiyo shida ilipoanza kwani hatujawasiliana naye kutoka wakti huo.

Kwa sasa niko na wapenzi wengine lakini ni lazima nimfikirie huyo mwanadada nikiwa nashiriki nao ngono ili niridhike. 

Sasa hii siri ningetaka niwatobolee hawa warembo wangu wote ili wajue wakati niko nao, kuna mmoja huwa nafikiria ili nimalize kazi. 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments