Toboa Siri: Niliua mtoto kuficha aibu kwani alikuwa wa baba wa kambo

mbusii na lion
mbusii na lion
Katika kitengo cha 'Toboa Siri' juma hili, watangazaji Mbusii na Lion walipigwa na mshtuko baada ya mwanadada mmoja kusimulia kisa kilichomkumba akiwa angali mtoto mdogo.

Alisimulia kuwa mamake aliolewa na mwanaume mwingine akiwa mdogo na kuwa hakujua kuwa yule baba wa kambo angegeuka kuwa mnyama kwake.

Kulingana na mwanadada yule, siku moja yule jamaa alimnajisi na kumtishia kuwa atamuua kama angemweleza yeyote kuhusu unyama huo, Isitoshe aliendeleza unyama ule kwa siku kadhaa na mambo yaliharibika baada yake kupata mimba.

Hapo alingoja hadi mtoto azaliwe na akaamua kuchukua sheria mkononi mwake na kumuua yule mtoto kwa kumnyonga ili kuficha ile aibu ya baba wa kambo. Cha kushtua ni kuwa hajawahi eleza yeyote kuhusu kisa kile na alingoja hadi kutoboa siri yake hewani.

Soma usimulizi wake na kisha uskize kanda yake.

Sasa mamangu aliolewa akiwa na mimi na mzee wake ambaye ni baba wa kambo wangu, aliniita siku moja na kuniambia nimpelekee simu kutoka kwa bedroom.

Sasa kwa ajili nilikuwa mtoto mdogo wa darasa la saba akanibaka na akaniambia nisimueleze yeyote kwani atanimaliza. Wawili hao bado wameoana.

Alinibaka karibu mara tatu hadi nikashika mimba yake na mamangu alidhani kwamba nimepata ile mimba huko nje, na nilishindwa kumwambia mamangu lakini ile siri ilikuwa inaniumiza moyoni.

Baada ya miezi tisa nikazaa kama kawaida na ilibidi nilimmaliza yule mtoto kwani singeishi naye. Nilimnyonga tu ivo na hata hawakujua chenye kilikuwa kinaendelea. Walimzika na hiyo kitu ikaishi lakini naangalianga huyu mzee nahisi kumfanyia kitu kibaya lakini sijawahi ambia mtu yeyote.

Alisimulia mwanadada ambaye alitoka kule na kusafiri hadi Nairobi.

Skiza kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be