Tofauti zilizopo baina ya rais na naibuye si za kutatuliwa rahisi - Murathe asema

Naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe amesema tofauti zilipo baina ya rais Kenyatta na naibuye William Ruto haziwezi kutatuliwa rahisi kamwe namna watu wanavyodhani.

Akiwa kwa mazungumzo na televisheni moja ya humu nchini, Murathe amesema Ruto amekuwa akipiga vita rais Kenyatta hata katika vikao vya seneti vilivyofanyika katika Ikulu.

Ameongeza kuwa Ruto alikuwa anawakatasa baadhi ya maseneta kukosa kuhudhuria mkutano huo katika jambo lililoonekana kama kumdharau kwa mkuu wa chama hicho.

“It is not a secret, the DP was actively whipping Senators not to attend. That is the height of insolence, it is unheard of anywhere in the world. That actually is not only defiance but a threat to the President.,” Murathe amesema

Wakati uo huo Murathe ametupilia mbali madai kuwa wabunge wanaoegemea upande wa kiongozi wa taifa walikuwa wanapania kumbandua mamlakani Ruto.

“This impeachment talk, I can tell you, is not on a card on the table. But as I had stated in an earlier interview, he should be careful with what he wishes for,” aliongezea Murathe.

Murathe amesema kuwa iwapo hatua ya kufanyia marekebisho baadhi ya viongozi wao itapelekea jaribio la kumg'atua mamlakani rais Kenyatta, swala hilo haliwezi kufanikishwa kwani wana idadi kubwa ya viongozi wanaomuunga mkono rais.

“If they want us to go there, I believe there are enough grounds,” amesimulia Murathe.