Toka Hapa! Mike Sonko afurushwa jukwaani Kabarak wakati wa mazishi ya Mzee Moi

sonko ejected (1)
sonko ejected (1)
Gavana wa Nairobi Mike Sonko  amefurushwa kutoka jukwaa kuu huko Kabaraka wakati maazishi ya rais Mstaafu Daniel Moi  yalipokuwa yakiendelea . Maafisa wa usalama  walimzuia Sonko kwenda katika  sehemu ambayo viongozi wengine walikuwa wamekaaa .

Haijabainika mbona gavana huyo wa Nairobi alizuiwa kuingia katika jukwa kuu .Alionekana amesimama pembeni kwa dakika kadhaa .Afisa moja alionekana akimueleza mbona hakuakiwa kufika katika eneo alilotaka kuketi . Sonko baadaye aliruhusiwa kuhudhuria hafla hiyo lakini akaketi na wakaazi .