Toka Nenda zako! Mastaa waliowahi kufukuzwa vilabuni

Asante ya Punda ni mateke na hivi sasa kocha mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane anampiga mateke Gareth Bale. Kunao wakali walio sajiliwa na vilabu vyao na kuwaletea mashabiki wa vilabu hivyo furaha mwanzoni ila mwishowe walijipata kwenye njia panda kwani walilazimishwa kufunganya virago vyao na kwenda zao.

Mashabiki, wachezaji wenza na hasa makocha wao walikuwa kwenye mstari wa mbele kuwafukuza.

Diego Costa

Mhispaniola huyu alisajiliwa na klabu ya Chelsea akitokea Atletico Madrid ya Uhispania mwaka 2014 na kocha Jose Mourinho.

Diego aliibuka kuwa kipenzi cha mashabiki ugani Stamfod Bridge huku akiisaidia Chelsea kunyakua taji la ligi kuu Nchini Uingereza mara mbili pamoja na taji la Fa.

Hata hivyo, ujio wake Antonio Conte ulimlazimisha Costa kufunganya virago vyake na kurejea nchini kwao Uhispania kwani Kocha huyo alisema hadharani kuwa hamhitaji costa kwenye kikosi chake. Kwa sasa Costa anachezea Atletico Madrid.

Gareth Bale

Gareth Bale kwa sasa analazimishwa kufunganya virago vyake pale ugani Santiago Bernabue na kocha mkuu Zinedine Zidane. Zidane amesema hadharani kuwa hamhitaji Gareth Bale msimu ujao huku kukiwa na kila dalili kuwa Bale angetamani kuendelea na maisha ya La liga.

Kwa sasa inangojewa tujue mahali Gareth bale atatimkia huku ikidaiwa kuwa huenda akarejea Uingereza ama atokomee Uchina.

Mauro Icardi

Muargentina huyu alipatana na jinamizi kutoka kwa mashabiki wake pamoja na Kocha ake msimu uliopita. Mashabiki wa Inter Milan walimkejeli Icardi mwezi Februali mwaka huu.

Lucianno Spalleti aliyekuwa Kocha wa Inter Milan, alisema hadharani kuwa Mauro Icardi hafai kuwa mchezaji wa Inter Milan Jambo lililofanywa hivi majuzi na kocha Mpya wa Inter Milan Antonio Conte. Kwa sasa Conte anatarajia kusajili Romelu Lukaku jambo litakalo mlazimisha Icardi aigure Milan.

Yaya Toure

Pep Gurdiola huenda akawa ndiye kocha bora duniani pia yeye alihusika kwa kumfukuza Yaya toure mara mbili maishani mwake.

Yaya Toure akichezea Barcelona Mwaka 2010, alikumbana na simba mkali kwa jina la Pep Gurdiola. Pep alimwambia hadharani kuwa hampendi wala hawezi kumpanga kwenye kikosi chake.

Yaya Toure alitimkia ugani Etihad. Mwaka 2016, Pep Guardiola alitia sahihi mkataba na Manchester City jambo Toure kufuganya virago vyake na kuondoka Manchester City.

Samuel Eto'o

Mshambulizi huyu tokea taifa la Cameroon alifukuzwa na Pep Gurdiola akiwa klabuni Barcelona mwaka 2009. Eto'o alisimulia jinsi Gurdiola alimnyanganya jezi na kumkosesha amani hadi ikamlazimu ahamie Inter milan.

"Gurdiola aliniongelesha mara mbili msimu mzima huku mara nyingi akinizungumzia kwa vidole jambo lililo nikosesha amani hadi kunibidi nihamie Inter Milan."