'Tongozeni kina dada kwa heshima na utaratibu,' Uhuru

Uhuru-
Uhuru-
Rais Uhuru Kenyatta amewarai vijana kuwatongoza kina dada kwa upole na  kukoma kusababsiha vurugu zisizofaa." Tongozeni  wanamke bila kuwadharau," Rais Uhuru Kenyatta amewashauri wanaume.

Uhuru amesema hayo wakati alipozindua rasmi mradi wa ujenzi wa  barabara ya JKIA-Westlands Jumatano.

Uhuru alitoa maoni hayo Jumatano kwa kile kilichoonekana kuwa majibu ya machafuko yaliyotokea katika bunge la Jiji  la Nairobi wakati spika Beatrice Elachi alirejea bada ya kipindi kirefu katika Bunge.

"Wazee waheshimu akina mama.. sio kuenda na kukosea mwanamke heshima...wewe enda umtongoze pole pole.. ukibahatika sawa..ukikosa tafuta mwingine" rais Uhuru alisema.

"Na hiyo ndio njia ya kumaliza ukabila lakini si kukosea mtu heshima..tunagombania nini..kushindana ni sawa lakini kuishi ni pamoja.." he said.

Uhuru alisema hayo alipozindua rasmi barabara ya JKIA-Westlands ambayo itakamilika baada ya miaka miwili.

Bunge la jiji la Nairobi liligeuka uwanja wa vita na machafuko n kwa masaa matatu baada ya Elachi kurejea bungeni.

Mali iliharibiwa, vifaa vya simu viliibwa wakati wafuasi wa Elachi na wapinzani wake walipkabiliana hadharani kwenye majengo ya bunge hilo.