Toto saafi! Kutana na kipusa mkorino ambaye ameziteka nyara nyoyo za wanaume wa Kenya (Picha)

Carey Priscilla,  mwanamke mkorino nchini amekuwa akiwapa  wengi usiku mrefu kwani urembo wake unazichana fikra zao na kuwaacha hoi .

Carey  ambaye ni  mtaalam wa kuwapodoa watu  na kuwarembesha  amekuwa akifanya kazi na 'macelebs' wengi nchini lakini sasa mtindo wake wa mavazi na miondoko yake mitandaoni imemfanya kujipa nafasi pia kama 'celeb'. Amekuwa akifanya uigizaji na pia ni model .

Licha ya imai yake ambayo wengi wanaitazama kuwa yenye maadili makali ya kiroho,  Carey amevunja mipaka ya mafanikio yake. Katika kazi yake yupo katika kundi la walio kileleni na iwapo ulikuwa unamtafuta msanii wa 'make up' basi umepatana na fundi wa wote .

Carey pia amefahamika kwa  kuendeleza  miundo ya mavazi ya kisasa na picha zake katika mitandao ya kijamii zinatoa  taswira ya mapenzi yake kwa fani ya fasheni. Hapa tazama msururu wa picha zake zikupe kasi ya moyo .