Tottenham wanapigiwa upatu kumsajili Philippe Coutinho

Tottenham wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho kwa mkopo wa msimu mmoja.

Raia huyo wa Brazil amehusishwa na vilabu kadha vya ligi ya Premier. Coutinho alifurahia mkopo wa miezi 6 chini ya Mauricio Pochettino alipokua meneja wa Espanyol mwaka wa 2012, akifunga mabao 5 katika mechi 16.

Inaaminika kuwa ni timu chache tu ndio zina uwezo wa kufikia gharama ambayo Barca's imemwekea Coutinho baada ya kulipa pauni milioni 142 January mwaka 2018. Kuwasili kwa Coutinho Tottenham kutaongezea fununu kwamba Manchester United wanatathmini kumsajili Cristian Ericksen.

Romelu Lukaku amesalia Ubelgiji licha ya Manchester United kumtarajia Carrington jana. Lukaku amekua ubelgiji akifanya mazoezi na Anderlecht kwa ruhusa ya United, lakini uamuzi huo ulikua wa jumatatu tu ambayo ni siku ya mapumziko ya mshambulizi huyo.

Vilabu vya Italia Juventus na Inter Milan vimekua vikimtaka mchezaji huyo wa miaka 26 msimu huu wa joto lakini havijafaulu, huku United ikimpa thamani ya pauni milioni 79.

United wamekataa ofa ya Inter Milan ya pauni milioni 68 na hivyo kuongeza uwezekano wa raia huyo wa Ubelgiji kusalia  Old Trafford.

Timu ya voliboli ya kinadada imewekwa katika kundi B katika michuano inayokuja ya All Africa Games itakayoandaliwa jijini Rabat, Morocco kuanzia Agosti tarehe 20 hadi 30. Malkia Strikers ambao ni mabingwa watetezi watakabana na mahasimu wao Cameroon, Senegal na Algeria katika kundi hilo.  Kundi A linajumuisha Morocco, Botswana, Mauritius na Nigeria.