Trouble ni Amani: Mudavadi sio kinara wa chama cha ANC Osotsi

pjimage
pjimage
Mbunge mteule Godfrey Osotsi  amesema  Musalia Mudavadi sio tena kinara wa chama cha ANC  na hakuna msukumo kutoka nje ili  kuleta mafarakano chamani humo.

Osotsi,  amesema  Mudavadi na maafisa wengine katika uongozi wa chama hicho wapo afisini kinyume cha sheria kwa sababu muda wao wa kuhudumu umekamilika na kusalia kwao uongozini ni ukiukaji wa katiba ya chama hicho.

“ Kama ilivyo sasa ANC hakina kiongozi wa chama. Mudavadi ameshakamilisha muda wake katika nafasi hiyo, ujumbe huu ni bayana’  amesema  Osotsi.

Osotsi  alikuwa akijibu madai ya kundi moja la viongozi wa ANC kutoka Migori waliodai kwamba anatumiwa na kinara wa ODM Raila Odinga kuzua mgawanyiko katika chama cha ANC.