True or False? Willis Raburu na mkewe Marya Prude watengana – duru zaarifu

Mtangazaji wa Citizen Willis Raburu na mkewe  Mary Ngami aka Marya Prude  hawaishi pamoja kwa mujibu wa  taarifa iliyochapishwa na  tovuti ya mpasho .

Inadaiwa  wawili hao walitengana mwezi mmoja uliopita. Duru zinasema  wawili hao walianza kupata matatizo baada ya Prude kugundua kwamba mume wake alikuwa na mahusiano ya pembeni. Inadaiwa wawili hao walikuwa wakiishi katika mtaa wa Phenom kabla ya kuihama nyumba yao .

 

“ Mwezi machi mambo yaligeuka na kuwa mabaya wakati raburu alipomnyaka mkewe kuondoka. Sasa anaishi kileleshwa na mwanamke mwingine."

Kidudumtu aliyetoa ufichuzi huo amekiri kwamba mkewe Raburu anaishi katika nyumba ya kukodi katika eneo la  Thindigua, Kiambu

“ kilichofanyika ni kwamba waligawana vitu vya nyumbani. Baadaye Raburu akampangishia Marya Nyumba   na kulipa kodi ya miezi miwili

Marya amefuta akaunti zake za mitandao ya kijamii. Wakati wa mwisho Raburu kuweka mtandaoni picha ya mkewe ilikuwa siku ya kuwaadhimisha  mama duniani .

Raburu  alifunga ndoa na Marya miaka miwili iliyopita  ambapo ni jamaa na marafiki wa karibu ndio walioalikwa pekee. Mapema mwaka huu, wawili hao walipoteza mtoto wao  ambaye bado hakuwa amezaliwa wakati Marya alipokuwa mja mzito .

Mpasho imesema ilipojaribu kuwasiliana na Raburu, hakujibu lolote juhudi zao za kuwasiliana na Marya pia zimeambulia patupu.