unnamed__1566971851_42090

Tsunami ya Raila kufagia wabunge wa TangaTanga. Ruto aidharau Tsunami

Baada ya kiongozi wa chama cha ODM Raila Amollo Odinga kutangaza kuwa uungwaji mkono wa mapendekezo ya BBI utawafagia kama upepo mkubwa wanaoipinga wakiwemo wabunge wanaohusishwa na kikundi cha TangaTanga, naibu wa rais William Ruto jana ametokea kuipuuziia mbali kauli hiyo.

Akiielezea kama Tsunami, Raila alitangaza kuwa Ruto na kikosi cha TangaTanga watabumburushwa na upepo huo mkali wa kisiasa na kubwagwa katika bahari.

Soma hapa:

Ruto hachelei! amrejeshea Raila makombora ya siasa za katiba

“Nimetazama angani na kuona mawingu yametanda,”Raila alihutubia wananchi waliojawa na furaha mtaa wa Kibera

“Ni ishara kuwa mvua itanyesha muda usio mrefu. Kuna upepo mkali unaovuma kutoka mashariki kwenda magharibi, kaskazini kwenda kusini. Utavurusha uchafu wote wa TangaTanga baharini.”alisisitiza kinara wa upinzani.

TangaTanga ni kikundi kinachohusika kumpigia debe na kumuunga mkono naibu wa rais.Hali kadhalika, Kieleweke ni kikundi kinachounga mkono lengo kuu la kuunga mkono BBI na kuhakikisha ajenda kuu za Rais Kenyatta zimetimia.

Ruto ameipinga BBI huku wanaomzunguka wakisema kuwa Raila anatumia “Handshake” yake na Rais Kenyatta kusambaratisha ndoto za Ruto kuwania urais mwaka ujao wa 2022.

Soma hapa:

Harmonize na Konde Gang ni biashara za lebo ya Wcb. Balaa kubwa kwa Kondeboy

 Ruto sasa anasema kuwa mpango wowote wa kubadilisha katiba ni mjadala unafaa kuwaleta wakenya wote pamoja bila kusababisha makundi pinzani. Akihutubia wananchi Kapsabet, Ruto amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba hayafai yasababishe mgawanyiko, chuki na hali ya wasiwasi nchini.

“Viongozi wengine waache vitisho. Hatutakupatia nafasi ya kugawanya nchi hii. BBI ikileta mapendekezo yake tutajihusisha katika mjadala.Hatutakubali Tsunami kugawanya nchi hii.” Alisema Ruto.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments