You tube ,mtandao wa wakora Asema Nandy

NA NICKSON TOSI

Nandy msanii tajika wa nyimbo za kizazi kipya tokea Tanzania amekashifu hatua ya baadhi ya watu kupunguza idadi ya watu wanaofwatilia nyimbo zake katika mtandao huo kila anapofanya wimbo mpya.

Nandy hivi maajuzi alitoa wimbo mpya ambao anasema ulikuwa na watu wengi waliokuwa wanautazama katika mtandao wa You tube na ilikuwa imesalia idadi kidogo tu wimbo huo uweze kuweka rekodi ya kufikisha watu milioni moja walioutazama, lakini kufukia majira ya usiki ,alishtuka alipoona idadi hiyo imepungua kwa kile anachosema ni watu kutaka kumwaribia taaluma yake ya usani.

Nandy ametoa wimbo mpya kwa jina Na Nusu ambao umefanya vyema katika Afrika mashariki.

''nimekuwa nikinyamazia swala hilo kwa kina kirefu,kuna vitu ambavyo vinafanyika katika mtandao wa youtube na sijui labda shida iko wapi,wakati video yangu inafikia watu alfu 900 walioutazama na kutoa maoni,kidogo tena idadi hiyo inapungua hadi 700 ama 800 alfu ya watu waliotoa maoni yao'alisema Nandy

NA NICKSON TOSI

Nandy alisema hataki kutaja majina ya watu ambao anawafahamu kama wanaohitilafiana na kupunguza idadi ya watu wanaotoa maoni yao kuhusiana na nyimbo ambazo akikariri kuwa haoni haja ya kufanya hivyo.

'Sitaki kutaja majina ya watu lakini nataka wanao husika na maswala ya usimamizi wa mtandao huo kuwa makini,manake maelfu ya wasanii wanapata hasara kutokana na tukio hilo.'alisema Nandy

Kwa sasa ,Nandy anatamba na wimbo mpya ambao unafanya vyema katika mitandao ya kijamii .