Mercy Masika and Massawe Japanni

Tukikwaruzana na mume wangu mimi ndio husema pole – Mercy Masika

Msanii wa nyimbo za injili, Mercy Masika hivi leo aliwapa wana ndoa, haswa kina mama changamoto alipofichua mbinu na siri yake ya kuhakikisha kuwa ndoa yake iko imara.

Aging like fine wine!The heart warming message Mercy Masika’s husband jotted down on her birthday

Kulingana na Masika ambaye anatambulika kwa nyimbo kama ‘Wema’ na siwezi jizuia, alifichua kuwa yeye ndiye huwa wa kwanza kunyenyekea na kuomba msamaha kila wanapokwaruzana na mumewe.

Akizungumza na mtangazaji Massawe Japanni katika kitengo cha ilikuwaje, Masika aliongeza kuwa alijifunza kuwa mnyenyekevu na hicho ndicho kimesaidia ndoa yake hadi wa leo.

Mimi ndio huwa wa kwanza kusema sorry. Alisema huku akiwashangaza waskilizaji wengi.

Niliambiwa na pastor wangu mwenye anasema sorry ndiye mkubwa, sababu bibilia inasema usilale kama mmekosana. Mimi nikilala kama tumekosana sijui naota ndoto gani, naota ndoto mbaya.

Mapenzi Yanarun Dunia: Mercy Masika And Hubby David Muguro Are Relationship Goals

Aliongeza akisema;

Uzuri mimi husahau haraka, hata tunaweza kosana na one hour upate hata sishikanishi vizuri. I think character yangu iko ivo kwa sababu mungu amenisamehea. I think na value sana neno la mungu kwa hivyo nikiona nakosea yaani naenda sana najikumbusha neno la mungu.

https://www.youtube.com/watch?v=sCI9mfaSG9M&feature=youtu.be

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments