Jackson Kibor

Tuko tayari kwa DNA! Wanawe Mzee Kibor wasema

Wanawe sita wa kiume wa  mfanyibiashara Jackson Kibor wamesema wako tayari kufanyiwa vipimo vya DNA ili kubaini iwapo ni watoto wake.

Kibor-compressed

Watoto hao wa Kibor walipoteza kesi kortini   ambayo Mzee Kibor alitaka wafurushwe kutoka shamba la la ekari 1200 huko Soy ,Uasin Gishu . Watoto hao wamesema wanafahamu kwamba baba yao mwenye umri wa miaka 88 anapanga kuwafanyia vipimo vya DNA ili kujua iwapo ni watoto wake kabla ya kuanza kuwagawia mali

Mahakama yakubali mzee kibor kufanyia wanawe DNA

Mmoja wao   Ezekiel Kipng’etich, amesema watakubali tu kufantyiwa vipimo hivyo katika taasisi ya serikali ambako matokeo  hayatabadilishwa kwa njia yoyote .

Mamake bwana  Kipng’etich’s , Naomi Jeptoo,  aliyetalakiana na mzee Kibor miaka miwili iliyopita aliunga mkono  msimamo wa mwanawe .

Ameongeza kwamba mwili wa mwanawe aliyezikwa katika shamba linalozozaniwa pia unafaa kufukuliwa ili kufanyiwa vipimo .

Bi  Jeptoo  amesema hadi leo hajaelewa mbona Mzee Kibor alitalakiana naye kwa sababu alikuwa muaminifu  kwa Mzee Kibor  tangu walipooana mwaka wa 1975.

Amesema iwapo vipimo hivyo vitafanywa kwa njia ya wazi bila muingilio wowote basi maisha ya wanawe yataboreka . amesema la kuficha  na anampenda Mzee Kibor licha ya tofauti kati yao .

Wosia wa Jackson Kibor kwenye Kongamano la Wanaume Eldoret

Mzee Kibor hata hivyo amesema yungali hajaamua wakati na eneo ambapo vipimo hivyo vitafanywa .Kibor alielezea masaibu aliyopitia  na Jeptoo na wanawe na hataki uhusiano wowote nao .

 

 

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments