Tukutane Mahakamani; ODM yaambia vyana tanzu vya NASA kuhusu fedha za vyama

MBADI
MBADI

Chama cha ODM kimejitokeza kujibu madai  ya vyama tanzu vya NASA kwamba vyama vyote katika muungano huo vinafaa kupata mgao sawa wa pesa za vyama vya kisiasa zilitengewa muugano huo na msajili mkuu wa vyama vya kisiasa.

Mwenyekiti John Mbadi ameambia vyama hivyo kwamba viko huru kupeleka malalamishi mahakamani.

Soma habari zaidi;

Mbunge huyo wa Suba Kusini, ambaye ni kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa alisema pesa walizopokea mwaka uliopita wa kifedha ni mgao wa ODM kulingana na idadi ya wabunge wake.

Mwenyekiti huyo wa kitaifa wa ODM alisema shilingi bilioni 4.5 walizopewa na mahakama ni za kati ya mwaka 2013-17 na wakati huo hapakuwepo muungano na chama cha ANC na kwamba chama kilichokuwepo kilikuwa UDF.

Alisema kwamba vyama vingine havikuwa na idadi ya wabunge inayohitajika ili kupata mgao wa pesa hizo.

“ODM imekuwa ikipokea pesa kama ODM. Ikiwa wanafikiria ODM imekuwa ikipokea pesa kwa niaba yao, wacha waende mahakamani. Hawa watu huzungumza bila ufahamu. Mahakama ziko wazi. Mbona wanazungumza tu kwa karatasi?” Mbadi aliuliza.

Soma habari zaidi;

Siku ya Jumatatu, naibu kiongozi wa ANC ambaye pia ni mbunge wa Lugari Ayub Savula alisema kwamba vyama tanzu vya NASA - ANC, MWiper na Ford Kenya pia wanastahili kupata mgao wa pesa hizo.

Savula pia alitaka pesa ambazo zilikatwa kwao kuendesha shughuli za muungano wa NASA kukaguliwa.

Mwezi Juni, kinara wa ANC Musalia Mudavadi alishtumu ODM kwa kukataa kugawanya pesa hizo kinyume na makubaliano ya vyama tanzu vya muungano wa NASA.

Soma habari zaidi;