Tulikuwa tayari kwa kifo cha Gavana Joyce Laboso, asema Abonyo

unnamed (5)
unnamed (5)
Edwin Abonyo amesema kuwa familia ilikuwa tayari kukubali kifo cha mkewe Joyce Laboso.

Hii ni baada ya mkewe kuugua saratani kwa muda mrefu.

Katika mahojiano na kituo hiki, Abonyo amesema kuwa mkewe alikuwa ameugua kwa mara ya pili.

"Ilikuwa wakati mgumu sana... ilikuwa mara yake ya pili..chances za kusurvive zilikuwa chini sana...tulikuwa tayari..."Kuhusu iwapo atazamia siasa, Edwin amesema kwa sasa hajapania lengo hilo,

Akisimulia kuhusu historia ya saratani aliougua mkewe, Edwin amefunguka kuwa gonjwa hili lilimpata mkewe miaka ya awali.

"Kwa mara ya kwanza kuugua ilikuwa 1991,kila mwaka alikuwa anapimwa kuona anavyoendelea..."

Kuhusu siasa kama mchezo chafu, Abonyo amekana dhana hiyo,

"Siasa sio mchezo mchafu...wanasiasa hapa kenya wanacheza mcheza mbaya...'

Kuhusu jinsi mkewe alivyoingia katika siasa, Abonyo amesema kuwa Laboso alizamia siasa kiajali tu.

"Joyce aliingia siasa kiajali tu...wakati huo alikuwa mhadhiri chuo kikuu cha Egerton..."

"Tulikuwa na network kwa ground na huruma ya wapiga kura..."

 "Mara ya pili alifanya kazi nzuri na kuenda bunge akateuliwa kuwa spika..."

"Siasa yake ilikuwa safi sana. Mimi hata hajawahi kunikubalia nichukue tender yoyote kwa seriikali ya kaunti..."

Kuhusu iwapo atazamia siasa, Edwin amesema kwa sasa hajapania lengo hilo,

"Yangu itakuwa ngumu sana. siasa za kenya zina misingi ya ukabila..."

"Sijafikiria sana na sijasema siwezi..." Abonyo