'Tulimueleza hali ya kisiasa humu nchini,' Junet Mohamed azungumza baada ya kumtembelea Raila Odinga

FRSk9kpTURBXy9lYjNmNDNhZWYxZDk4MGRjYjFiMzFjMzc1Y2E3YTdkNy5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
FRSk9kpTURBXy9lYjNmNDNhZWYxZDk4MGRjYjFiMzFjMzc1Y2E3YTdkNy5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed Alhamisi jioni alizungumza baada ya kumtembelea kinara wa chama cha ODM Raila Odinga nchini Dubai.

Raila alisafiri kwenda nchini Dubai ili kupokea matibab mwezi jana.

Junet ambaye alisafiri na gavana wa Mombasa Hassan Joho alisema kuwa kinara huyo anazidi kupona baada ya upasuaji aliofanyiwa nchini humo.

Pia alifichua kuwa walizungumzia mambo ya kisiasa, kwa muda na kinara Raila Odinga, Junet alikuwa na haya ya kusema,

"We met him and he was in high spirits. We had tea together and briefed him about what is going on back at home. He told us he was eager to be back home. We updated him about the political situation in Kenya and we laughed together." Alizungumza Junet.

Junet na Joho walisafiri kwa ndege ya kibinafsi huku wakiibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya mkoba wa mwanamke kuonekana kwa picha walizoposti wakiwa kwenye ndege hiyo.

Alhamisi wanamitandao walikuwa na mjadalaa huku wakijadili haswa mkoba huo ni wa nani, huku wengi wakisema kuwa ni wa Betty Kyallo ambaye alikanusha madai hayo.