Tulipeni milioni moja ili tuwachilie Arteta! Man City yaagiza wanabunduki

arteta
arteta

Manchester City wanataka walipwe pauni milioni moja ili wavunje mkataba na kocha wao msaidizi Mikel Arteta - Arsenal wanataka kumtangaza Arteta kama kocha wao mkuu mpya. (Mail)

Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 23, baada ya kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Japani na klabu ya Red Bull Salzburgforward Takumi Minamino, 24. (Star)

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amedai kuwa Spurs "hawaogopi" kumuuza kiungo mchezeshaji raia wa Denmark Christian Eriksen, 27, kwa timu pinzani za England mwezi ujao. (Evening Standard)

Carlo Ancelotti anatarajiwa kutangazwa kama kocha mpya wa Everton baada ya kusaini mkataba wa pauni milioni 11.5 kwa mwaka. (Mirror)

Juventus wanatarajiwa kumbakiza beki wao raia wa Uturuki Merih Demiral, 21, licha ya klabu kadhaa za ligi ya Primia na pia AC Milan kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (Calciomercato)

Paris St-Germain wanatarajiwa kusuka mipango ya kumsajili Pep Guardiola kama mbadala wa kocha wao wa sasa Thomas Tuchel. (Le 10 Sport via Daily Mail)

Winga Mjerumani Leroy Sane, 23, anataka kuhamia miamba ya nyumbani kwao Bayern Munich na anapiga hesabu za kuihama Manchester City mwezi Januari. (Bild via Mirror)

-BBC