'Tuliuzwa na tukakubali, usisahau kwa nini baba alikuchagua kuwa katika kamati hii -Moses kuria amwambia Otiende Amollo

Mbunge wa Gatundu Moses Kuria amemuuliza mbunge wa Rarieda Otiende Amollo asisahau kwa nini alipewa nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kamati ya sheria bungeni na kinara wa ODM Raila Odinga.

Kupitia katika ujumbe wa kumpa hongera na viongozi wengine waliochaguliwa kuwa katika kamati hiyo, kuria alidai kuwa viongozi hao walichaguliwa ili kupeana ripoti kuhusu Building Bridges Intiative(BBI).

Wengine waliochaguliwa kuwa katika kamati hiyo kutoka kwa chama cha ODM ni Mbunge wa Suna Junet Mohammed, mbunge wa Homa Bay Peter Kaluma na mbunge wa Mathare Anthony Oluoch.

Moses Kuria pia aliwakumbusha wanapswa kuzingatia agenda za kamati hiyo;

“Congratulations Hon Otiende Amolo incoming Chair of the Justice & Legal Affairs Committee. Congratulations Hon Junet Mohammed, Hon Peter Kaluma and Hon Anthony Oluoch for making it to this vital committee. Now do not forget why Baba has appointed you to this vital committee- Deliver BBI, deliver a Baba friendly Chief Justice, deliver a Baba compliant IEBC and a Baba nominee for the Registrar of Political Parties. Stick to your Terms of Reference (ToRs) and Key Performance Indicators (KPIs). Tuliuzwa na tukakubali. Ilibidi." Aliandika Kuria.

Chama cha Jubilee awali kimekuwa kikifanya mabadiliko katika chama hicho na hata wengine kupoteza vvyeo vyao.