"Tumezuiwa kuingia kwa kaburi la bwanangu.." Mkewe bilionea Reginald Mengi alia

reginald mengi
reginald mengi
Reginald Mengi ni bilionea kutoka Tanzania na ambaye aliaga dunia mwaka uliopita huku akimuacha mke, Jacqueline Mengi na watoto wawili.

Hapo awali, Jacqueline Mengi alikuwa msanii aliyetambulika kwa jina K-Lynn.

Jacqueline amewashangaza wengi pale alipofunguka na kukiri kuwa anazuiwa kutembelea kaburi la mumewe.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, aliandika;

Nimenyamaza kwa mengi sana tu. Mmefikia hatua ya kunizuia mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu, tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na Baba wa watoto wangu! Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya.

Mumewe bwana Mengi, aliaga dunia mnamo taraehe 2, Mei, 2019 akiwa na umri wa miaka 75.

Alikuwa tajiri mkuu aliyemiliki kampuni kadhaa za uanahabari pamoja na kampuni zingine Tanzia kote.

Mengi pia alikuwa mwandishi na aliandika kitabu kwa jina, I can, I will, I must.

Kabla ya kumuoa Mengi, bi Jacqueline aliwahi shinda taji la Miss Tanzania. Anajulikana kwa ngoma zake "Crazy over you, "Nalia kwa furaha " na nyinginezo.