Tumia curfew vyema! Njia 10 za kukusaidia kupunguza mafuta mwilini

Mara yingi sababu ambazo sisi hupeana ama hutumia inapofika ni wakati wa kutunza miili yetu ni za kustaajabisha, hata hivyo nitasema kuwa zingine zinaeleweka.

Kusema ukweli, hakuna vile utamshawishi mwanafunzi ambaye huenda darasani jioni au mama aliye na mtoto mchanga apate muda jioni kufanya mazoezi.

Kitakachofuata ni vijisababu chungu nzima, mara wana kazi ya kumaliza, lakini swali ni je, na muda huu wote wa curfew au karantin, sababu yako ya kutofanya mazoezi itakuwa ipi?

Wengi wetu, vijana hadi wazee tunajaribu kila tuwezalo ili kuhakikisha miili yetu ik0 kwenye shepu tunazopendelea na tunafanya hili kwa kuchoma mafuta mwilini.

Wengi hulaumu marafiki wao huku wengine wakilaumu kazi zao ambazo huwazuia kufanya mazoezi, lakini wakikosa kuutumia muda huu wote, mambo yakirudi kama zamani watamlaumu nani

Hata hivyo, nilibahatika kupatana na orodha ya njia 10 za kukusaidia kupunguza mafuta mwilini.

  1. Punguza kiwango cha sukari unachotumia
  2. Jaribu kutumia mafuta ambayo yana afya
  3. Usile kiwango kingi cha ugali, mchele au pia mkate 
  4. Kunywa angalau lita mbili au tatu za maji kila siku
  5. Jifunze jinsi ya kupambana na stress
  6. Ongeza viwango vya mboga kwa chakula chako kama vile sukuma wiki au spinach
  7. Kula protini
  8. Jaribu kusongesha mwili wako kila unapopata wakati kwa mfano, kusakata ngoma, kuogelea au pia kutembea mara kwa mara.
  9. Jaribu kunywa maji moto yenye limau mara kwa mara
  10. Upende mwili ulio nao huku ukijaribu kuifanyia kazi na kuuboresha