Tumkimbilie Mwenyezi! Willis Raburu awarai wakenya

Mwanahabari Willis Raburu ambaye alisema zaidi baada ya kutengana na mkewe, sasa amewahimiza wakenya kusalimisha shida zao zote kwa Mungu haswa wakati huu ambapo watu wengi wanakumbwa na changamoto nyingi.

Amehimiza kila mmoja kujitathmini haswa wakati huu ambapo makanisa na maeneo mengine ya kuabudu yamefungwa kutokana na virusi vya corona.

"Covid has really changed how church is done. The biggest realization I think should be that we are the church, not a building. Your personal relationship with God is what matters," alisema Willis.

Mwezi Februari mwaka huu,Willis alijikuta pabaya baada ya kudai kuwa imani yake kwa Mungu imeanza kudidimia baada ya kumpoteza mwanawe Adana.

Willis alishangazwa ni kwa nini Mungu alimwacha wakati alipokuwa anatarajia kupata mwanawe wa kwanza japo akafariki.