'Tunaendelea kupata nguvu na kuwa wanamageuzi kukabiliana na wakora wa kisiasa.' UJumbe wa Miguna kwa mkewe

Mwanaharakati matata Miguna Miguna Alhamisi Mei 14 aliwasisimua wafuasi wake mtandaoni baada ya kumsifia mpenziwe kutokana na jumbe zake zenye moto wa mageuzi, wengine wamekuwa wakimuona Miguna kama simba mkali jangwani.

Hawakukosea waliposema kuwa mapenzi yana run dunia, Miguna Miguna hujulikana kwa jumbe zake kali za wanamapinduzi na wafuasi wake wamekuwa wakimuona kama jenerali vitani.

Miguna alhamisi wiki hii amewaonyesha wengi kuwa pia naye ni inadamu na ana hisia na kuwa kuna wakati hufika anazama kwenye mapenzi.

Wengi wamekuwa wakishangaa iwapo ndume huyo mwenye ulimi wenye moto ana familia na huishi nao vipi.

Aidha, hata maswali huibuka iwapo ndume huyo ana uwezo wa kutulia na kumpa mwanadada yeyote maneno matamu. Lakini Miguna aliwaonyesha wengi kuwa yeye pia ni gwiji katika ulingo wa kuwanasa mabinti wazuri.

Kupitia mitandao ya kijamii Miguna alimwandikia mkewe ujumbe mtamu alipokuwa anasharehekea siku yake ya kuzaliwa.

"Furahia siku ya kuzaliwa mrembo wa Gem, wewe ndiye mama wa kwangu na watoto wangu. Tunaendelea kuwa wachanga, kupata nguvu na kuwa wanamageuzi kukabiliana na wakora wa kisiasa." Aliandika Miguna miguna.

Wawili hao wana watoto watatu na wamekuwa wakiishi nchini Canada huku ikiwa wazi Miguna hufurahia penzi lake, ni wazi kuwa miguna pia anaweza tamka maneno matamu kwa mwanadada.

Picha ya mkewe inaashiria kuwa Miguna kwa kuchagua warembo si kidogo bali ni mkali katika sekta hiyo pia kama vile ni mkali katika sekta ya kisiasa.