TUNZA MTOTO WAKO!Kizaaza katika boma la Kutuny baada ya mwanamke kudai fedha za matumizi ya mtoto waliyezaa naye

kUTTUNY
kUTTUNY
  Kulikuwa na patashika katika boma la  mbunge wa cherangany Joshua Kutuny mtaani Hardy wakati mwanamke mmoja alipowasili huko akidai kwamba mbunge huyo amemtelekeza mtoto waliyezaa naye .

Joyline Chemutai  anadai kwamba  mbunge huyo hajakuw aakituma pesa za kumsaidia mwanawe . Polisi wamesema walipewa taarifa kuhusu kizaazaa katika boma la mbunge huyo mwezi wa  saa sita usiku .

Polisi waliojibu tukio hilo walielekea kwa Kutuny na kumpata mwanamke huyo akipiga kelele . katika  patashika hiyo afisa mmoja wa polisi kwa jina Emmanuel Maiyo alifyatua risasi hewani ili kuleta utulivu .