''Tupatieni mwili wa mpendwa wetu''Familia yaomba uongozi wa mochari

Familia moja inayoishi kwenye nyumba ya udongo katika kitongoji duni cha Mwakio karibu na milima ya Shimba iliomba mochari ya Kijabe itoe mwili wa mpendwa wao waizike kwani mpendwa wao hafai ukatili huo.

Hata hivyo, hospitali imekuwa ikikataa ombi hili na kusema kuwa, haiwezi kubali kuwapa mwili huo wauzike kwani hawajamaliza kulipa bili ya mochari.

Mwili huu wa Samson Munyao umeshikiliwa kwenye mochari ya Kijabe kwa muda wa miezi miwili na kila siku, bili huongezeka kwani bili ya siku moja ni 2,700.

Familia hii iliuza mali yao yote ili waweze kulipa deni ho na kumzika marehemu Samson lakini hawakufaulu.

Zaidi ya hayo, familia hii ilijaribu kuwa na harambee za kuchanga hela hizi lakini bado pesa walizozipata hazikutosha kugharamia bili hii.

Mjane Faith Samson alisema kuwa, walijaribu kuongea na wamudu wa mochari ya Kijabe waweze kuwapa mwili wao wauzike kisha walipe bili hiyo baadae lakini wakakataa.

Cha kusikitisha pia ni kuwa gharama inaendelea kuongezeka

''Tulijaribu kuwaomba wamudu watupe mwili wa mpendwa wetu lakini wakakataa kutuoa mwili wetu na kutumbia tutafute pesa haraka kwani, tunapozidi kukaa bila kulipa, bili inazidi kupanda.'' Alisimulia vyombo vya habari.

Munyao alipata tatizo la kutembea mwezi wa nane mwaka uliopita na ugonjwa huu ukazidi  mwezi wa kumi mwaka huo huo na ndipo akapelekwa kwenye kliniki ya Mombasa .
Mwanamke huyu alisema kuwa, mme wake alipata ugonjwa wa mapafu (Pneumonia) alipokuwa hospitalini na hakuwa anaweza kupumua vizuri na ata wakati mwingine alikuwa anazimia.
 ''Baada ya kliniki, mume wangu alipata Pneumonia, mapafu yake yalikuwa yanafura, hakuweza kupumua na sazingine alikuwa anazimia.'' Mjane Faith alisema.

Munyao alipelekwa kwenye hospitali ya Msambweni kupimwa na bili ikawa elfu 300,000 lakini hata baada ya kupimwa, hakupata afueni.

Familia hii iliuza shamba na mifugo ili waweze kupata hela za kuenda hospitali ya Pandya Memorial  jijini Mombasa.

Wataalamu walisema kuwa, uti wa mgongo wa Munyao ulikuwa  umevunjika kwenye uti wa shingo ndipo akapewa ushauri aende AgaKhan hospital kufanyiwa upaswaji ambao iligharimu  shilingi 450,000.

Mwezi wa nane tarehe nne, Munyao alipelekwa kwenye hospitali ya Kijabe ambapo walilipa fee ya kusajiliwa ya elfu 300,000 na cha kusikitisha ni kuwa, Munyao alikata kamba wakati ambao familia yake ilikuwa inatarajia kuwa atapona.

Ndugu yake alisema kuwa, Samson hafai ukatili huo kwani marehemu Samson alikuwa mcha Mungu na jamaa aliyependwa na wote.

Familia yake ina matumaini kuwa siku moja wataweza kumzika mpendwa wao.