Tusaidieni! Familia ya Jowie Irungu yataka 3.5 Milion

Familia ya Joseph Irungu aka Jowie inahitaji msaada wa kuchangisha shilingi milioni 3.5  ili kumsaidia jamaa yao  anayehhitaji upasuaji wa bone marrow .

Akitumia  mitandao ya kijamii Jowie ambaye sasa anajiita  Kush Irungu  aliandika;

‘FAMILY COMES FIRST

AGNES NYAGUTHII IS IN URGENT NEED OF A BONE MARROW TRANSPLANT AND THE COST IS KSHS 3.5 MILLION.

WE KINDLY APPEAL TO ALL FAMILY AND FRIENDS TO ASSIST US RAISE THIS AMOUNT TO GIVE OUR MOTHER A BETTER FIGHTING CHANCE.

GOD BLESS YOU. MPESA PAYBILL NO: 714 4 015

ACCOUNT NAME: AGNES NYAGUNYAGUTHII.’

Jowie hajakuwa mitandaoni sana kama hapo awali baada ya kuachiliwa huru kwa bondi ya shilingi milioni 3 . Alikuwa jela kwa kipindi cha mwaka mmoja unusu kwa tuhuma za mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani. Baada ya kuachiliwa huru, Jowie aliamua kufanya marekebisho katika  akaunti  zake za  mitandao ya kijamii .

Alianza kwa kufuta picha zote  na kuziacha chache za ‘ marafiki wa kweli ‘ na familia .

Irungu sasa anaishi na wazazi wake nakuru  na huwa anaripoti kwa afisi ya chifu kila mwezi kama ilivyoagizwa na mahakama. Amefuta posti zake 16 zilizosalia na kuwafuta watu 289 huku mashabiki wanaomfuata sasa wakiwa 27.9k