Tutahakikisha somo la Rastafarian linafunzwa shuleni - Wambua

rastafarian
rastafarian
Jamaa aliyegonga vichwa vya habari alipolalamikia mwanawe wa kike kufukuzwa shuleni kwa 'kosa' la kuwa na nywele za dreadlocks, na kuwa kwa dini la ki Rastafari, bwana John Wambua amefunguka kuhusu dini hiyo.

Katika mahojiano ya moja kwa moja na Radiojambo.co.ke, Wambua alizungumza nasi, siku chache tu baada ya mahakama kuamua kuwa rastafarian ni dini na nywele zao ndefu ni mojawapo ya ishara za kiroho za dini hiyo.

Hii ni baada ya mwanawe msichana kufukuzwa katika shule ya upili ya Olympic kwa tuhuma za kuwa na nywele ndefu aina za dreadlocks.

Baada ya ushindi huo, Wambua anasema hatotulia kwani nia yao ni kuhakikisha Rastafarian imefunzwa shuleni kama dini.

Na feel poa kwa sababu kama korti imetu recognize inamaanisha tuna majukumu mengi ya kufuatilia, kwa sababu rasta ni mtu hajakuwa akitambuliwa kwa miaka mingi. Alisema Wambua.

Aliongeza,

Wengine wanatudharau, hawajui maana ya livity yetu na ni vizuri wakituheshimu kama hizo dini zingine pia, kama hiyo sekta ya elimu tulipigania tukafaulu.

Watoto wetu wakimaliza shule labda watanyimwa kazi kwa sababu ya hizo nywele na hiyo pia tunataka kumaliza.

Anasema kuwa alianza kupingana na mambo ya kanisa akiwa na umri wa miaka kumi hivi akisema kuwa alikuwa anaambiwa ana maswali magumu na mara waliokuwa wanamfunza dini walisema hataki kuskiza.

Nilikuwa nasoma kwa bibilia na nilipenda story ya Daudi vile aliua Goliath na mungu akamuahidi ufalme, sasa nilitaka kujua ilienda wapi kwani ya Malkia Elizabeth iko.

Alivyojiunga na kundi la Rastafarian.

Kwanza sikuwa napenda kunyolewa nywele na sikuwa natambua mimi ni rasta lakini u rasta ulikuwa ndani yangu. Nilikuwa nashikwa na shangazi wangu karibu wanne ili ninyolewe.

Anasema kuwa kuna wazee walioko duniani kote ambao huwafunzi njia za Rastafarians na wao hukutana Saturday ambapo husoma zaburi za mfalme Daudi.

Nilioa mtu ananipenda na nilikuwa nampenda, sikuwa na shida nyingi kwani alinipata nikiwa rastafrian na sahii pia yeye ni Rastafarian." Alisema akidai kuwa pamoja walipata watoto sita na wote ni wa dini hilo.