'Tuwachague viongozi wenye uadilifu' Ekuru Aukot asema

17268072_573588402836466_6933455341900267520_n (1)
17268072_573588402836466_6933455341900267520_n (1)
Katika mahojiano na Radio Jambo na Gidi na Ghost asubuhi hii leo, kiongozi wa chama cha Third way alliance, Ekuru Aukot alisema kuwa wakenya wanafaa kuwachaguwa viongozi wenye uadilifu.

Aliendelea kusema kuwa wakenya wanawachagua viongozi kisha wanalalamika baadaye licha ya kuwa ni jukumu lao kuwachagua viongozi wanaofanya kazi.

Aliendelea na kusema kuwa marais wanapochaguliwa wanapoteza wakati muhula wa kwanza wakiwafurahisha watu na kuanza kufanya kazi wakati wake unapodidimia.

Ekuru Aukot aliendelea kusema kuwa wanasiasa wanafaa kushughulikia kampeini ya punguza Mzigo na alieleza mambo ambayo yanahusika na Punguza mzigo ikiwemo ufisadi, kuongeza pesa nyingi kwa mishahara ya watu na mengineo.

Ekuru aliendelea na kufafanua kuwa kipindi ambacho kinarekebishwa ni cha urais pekee bali sio cha ugavana. Aliendelea kusisitiza viongozi kufanya kazi zao na kuwajibikia kazi zao.

Alisema kuwa wakenya wanachanga na kuunga mkono mswada wa punguza mzigo.

Soma mengi