Tuwashtaki wote wanaotoroka maeneo ya karantini-Mutahi Kagwe awaambia wakenya

EWNYH4GXQAAa30c
EWNYH4GXQAAa30c
NA NICKSON TOSI

Akitangaza idadi ya watu walioathirika na virusi vya Corona nchini kufikia watu 303 baada ya wakenya 7 kupatikana na virusi hivyo, waziri wa afya Mutahi Kagwe amewahimiza wakenya kuwa ange na kuwashtaki wakenya ambao wamekuwa na tabia ya kutoroka maeneo ambayo wamewekwa kwenye karantini.

Mutahi amesema kuwa maafisa wa usalama milioni 47 hawawezi kuwekwa kufuatilia wakenya miloni 47 ambao hawazingatii masharti ambayo serikali imeweka.

Yanajiri hayo watu 57 katika kaunti ya Meru wakiwa wametiwa mbaroni baada ya kukiuka agizo la serikali la kufumukana katika eneo moja.

Rais Uhuru Kenyatta alitilia podo usemi huo akisema mkenya atakayepatikana akikiuka amri atawekwa kwenye karantini ya lazima na wale wanaokimbia katika maeneo ambayo wamezuiliwa watachukulia hatua.