Tuzo za wachezaji bora wa kpl msimu wa 2018/2019

Francis Kahata anaongoza kwenye kinyaga'nyiro cha mchezaji bora wa msimu pamoja na kiungo bora wa msimu. Tuzo hizo ambazo huandaliwa na muungano wa wanahabari wa michezo humu nchini Kenya, (SJAK) zinatarajiwa kupeanwa siku ya jumatano wiku ijayo ndani ya Kenya National Museum.

Kahata anawania tuzo la mchezaji bora huku akitarajia ushindani mkali kutoka kwa Joash Onyango wa Gor Mahia, Enosh Ochieng wa ulinzi stars, Umaru Kasumba wa Sofapaka, Allan Wanga wa Kakamega Homeboyz pamoja na Boniface Michiri wa Tusker.

Katika awamu ya mlinda lango bora wa msimu, Farouk Shikalo aliyesajiliwa na Yanga anaongoza orodha huio hio huku wapinzani wake wakuu wakiwa ni Ndikumana wa Sofapaka,Kelvin Omondi wa Sony,Morgan Alube wa Chemelil pamoja na Adisa omar wa KCB.

Tuzo la mlinzi bora wa msimu linawaniwa na Haroun Shakava`pamoja na Joash Onyango wa Gor Mahia, Brian Otieno wa Bandari, Kelvin Wesonga wa Sony Sugar, Faina Jacob wa Sofapaka na mlinzi wa Kushoto wa Mathare United, David Owino.

Whyvonne Isuza wa AFC Leopards anatarajiwa kuwa mpinzani wake kahata kwenye tuzo la kiungo bora wa mwaka huku pia wakishuhudia ushindani kutoka kwa Abdallah Hassan wa Bandari, Cliff Nyakeya wa Mathare, Danson Chetambe wa zoo Kericho na Muchiri wa Tusker.

Tuzo la mshambulizi bora wa mwaka litang'ang'aniwa na Allan Wanga wa Homeboyz, David Majak wa Tusker pamoja, Jackson Dwang wa Nzoia Sugar, Nixon Omondi wa Kariobangi sharks pamoja na Joshua Nyatini wa Sony Sugar.
Aliyekuwa kocha wa Gor Mahia Hassan Oktay atawania tuzo la mkufunzi la kocha bora na Robert Matano wa Tusker, Francis Kimanzi aliyekuwa Mathare na Patrick Odhiambo aliyekuwa koacha wa Sony Sugar