Tyranny of jokers?Ruto aachwa mataani baada ya Maseneta wake kushindwa kumuokoa Kindiki

Naibu wa rais William Ruto  yupo katika njia panda kisiasa  baada ya matukio ya hivi karibuni ya kisiasa kuonyesha kwamba kuna pengo kubwa la idadi ya wabunge na maseneta wanaomuunga mkono .

Pengo hilo limeacha mwanya wa uwezekano wa DP Ruto kufurushwa kupitia kura ya kutokuwa na imani naye . Hilo limedhihirika baada ya maseneta  54 kupiga kura ya kuidhinisha kuondolewa wa Kindiki Kithure kama naibu wa spika wa senate  dhidi ya masenetya saba waliojaribu kuikoa kazi ya Kithure .

Kindiki ambaye ni profesa wa sharia na msomi tajika  amekuwa miongoni mwa   wafuasi sugu wa Ruto na wanaomuunga mkono kuchukua usukani kutoka kw arais Kenyatta mwaka wa 2022 na kuondolewa kwake kama naibu wa spika kutapiga pancha jitihada na ushaiwishi wake katika eneo la mashariki mwa  Mlima Kenya . Kwa wakati mmoja aliwahi kutajwa kama viongozi ambao huenda wakatumiwa na Ruto kama mgombea mwenzake katika uchaguzi mkuu ujao  na kuondolewa kwake kutakuwa pigo kwa kambi ya Ruto na kwa taaluma yake kisiasa .

Siku ya ijumaa maseneta 54 kati ya 67 waliidhinisha kura ya kumuondoa kindiki kutoka wadhifa huo .ni saba pekee ambao walipinga kura hiyo  na ni Kipchumba Murkomen wa Elgeyo Marakwet, Susan Kihika wa Nakuru, Samson Cherargei wa  Nandi, Aaron Cheruiyot wa Kericho, Christopher Lang'at wa  Bomet  na seneta wa Meru   Mithika Linturi. Maseneta wawili ambao  waliunga mkono kuondolewa kwa Ruto  ingawa hawaku bungeni wangezidisha idadi ya  wanaompinga Ruto kuwa 56 lakini kura zao hazikukubalika .

Hoja hiyo ilihitaji tu maseneta 45 ili kupitishwa .

Katika kinachoonekana kama kubadili msimamo wao ,maseneta watano wateule ambaop hapo awali walikuwa katika kambi ya Ruto  walimuacha na kupiga kura pamoja na maseneta wa mrengo wa rais Kenyatta na kiongozi wa Odm Raila Odinga  ambao waliunda ngome ya pingamizi dhidi ya Ruto .

Maseneta hao ni   Falhada Dekow Iman, Naomi Jillo Waqo, Victor Prengei, Mary Seneta Yiane a na  Millicent Omanga.