Tyson Fury ambandaua Wilder na kunyakuwa ubingwa wa WBC

Boxing - Deontay Wilder v Tyson Fury - WBC Heavyweight Title - The Grand Garden Arena at MGM Grand, Las Vegas, United States - February 22, 2020 Tyson Fury knocks down Deontay Wilder during the fight REUTERS/Steve Marcus
Boxing - Deontay Wilder v Tyson Fury - WBC Heavyweight Title - The Grand Garden Arena at MGM Grand, Las Vegas, United States - February 22, 2020 Tyson Fury knocks down Deontay Wilder during the fight REUTERS/Steve Marcus
Bondia Tyson Fury amembandua Deontey Wilder na kuwa bingwa wa WBC kwa uzani wa heavy weight jiji Las Vegas asubuhi ya leo.

Fury alishinda kwa knock out katika raundi ya 7 ya mechi hio, Wilder ambaye aliumia sikio kunako raundi ya tatu alizidiwa baada ya kuangushwa mara kadhaa. Raia huyo wa Uingereza alimpongeza mpinzani wake kwa pigano hilo, licha ya kupoteza huku kukiwa na matumaini kwamba watapigana tena hivi karibuni.

Mkusanyiko wa habari za spoti:

Mechi za Serie A katika eneo la Kaskazini la Italia Lampardy na Veneto zimesitishwa kutokana na mkurupuko wa Corona virus. Mechi hizo zilikuwa kati ya Inter Milan na Sampdoria, Atalanta dhidi Sasuolo na Verona dhidi ya Cagliari.

Hamna dalili za iwapo mechi hizo zitachezwa wakati mwingine baada ya serikali ya Italia kufunga taasisi zote za mafunzo na kupiga marufuku mikutano ya hadhara.

Ligi kuu nchini KPL inaendelea leo huku mabingwa watetezi Gor Mahia wakiwania kusalia kileleni na ushindi dhidi ya Zoo Kericho. Tusker nao wataalika Wazito huku wakitafuta alama tatu muhimu. Ulinzi Stars watapiga dhidi ya Kisumu All Stars nao Kakamega Homeboyz wakipambana na Chemilil sugar.

Katika ligi ya Uingereza Manchester United watacheza na Watford huku wakiwania kupanda hadi nafasi ya tano, nao Arsenal wakicheza na Everton. Wolves watacheza na Norwich huku kinyanganyiro cha kumaliza katika nafasi za nne bora kikiendelea.

Manchester City waliwanyanyua Leicester bao  1-0 Jana na kupanda alama 19 nyuma ya Liverpool.

Bao la Gabriel Jesus kunako dakika ya 80 lilitosha kuwapa Citizens ushindi na kupanda alama Saba juu ya the foxes ambao wako katika nafasi ya tatu, baada ya penalti ya Sergio Agguero kuokolewa na Kasper Schmeichel.

Wakati huo huo Chelsea waliwanyuka Tottenham 2-1 katika derby ya London ugani Stamford bridge na kumaliza msurururu wao wa kutoshinda mechi nne katika EPL. Mabao ya Olivier Giroud na Marcos Alonso katika kila kipindi yalihakikisha bao la Antonio Rudiger la kipindi cha lala salama lilikuwa tu la kuwaliwaza Spurs.

Huko Uhispania Lionel Messi alifunga mabao manne mabingwa Barcelona walipowanyuka Eibar 5-0 na kupanda kileleni mwa La liga wakiwa na alama 55 baada ya mechi 24.

Wakati huo huo Real Madrid walifungwa 1-0 na  Levante, na kushuka hadi nafasi ya pili alama mbili nyuma ya Barcelona kabla ya El Classico. Kwingineko Juventus walipanda alama nne juu ya Serie A baada ya ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Spal.

KCB walipanda hadi katika nafasi ya pili kwenye jedwali la KPL kwa ushindi 3-1 dhidi ya Posta Rangers jana. Bandari pia waliwapa kichapo Mathare United cha mabao 3-1 kocha Twahir Muhidin alipopata ushindi wake wa kwanza tangu kuchukua uskani wa timu hio ya pwani.

AFC Leopards waliendeleza matokeo mazuri chini ya kocha Antony Kimani walipowanyuka Sofapaka 2-1 na kupanda hadi katika nafasi ya 5 kwenye jedwali, huku Western Stima wakitoka sare tasa na Kariobangi Sharks.