Ubalozi wa Amerika sasa unakubali noti mpya unapolipia visa

pesa
pesa
Ubalozi wa Amerika hapa jijini Nairobi umesema sasa unakubali  noti mpya unapolipia visa pamoja na huduma zozote katika ubalozi huo baada ya kufanya mkutano na benki kuu ya Kenya.

Ubalozi huo umesema ulifikia uamuzi huo baada ya ushirikiano na benki kuu ya Kenya na kupewa vifaa pamoja na mafunzo yanayohitajika ili waweze kukubali noti hizo mpya.

Wakenya sasa wanaweza kulipia visa kwa kutumia noti mpya na za kale ambazo zitatumika hadi Oktoba 1.