’Viongozi imara huwa hawanyamazishi raia wao. Mataifa yanayokuza demokrasia huwapa wananchi uhuru wa kuongea na kuikosoa serikali”
Kitendo cha kumtia nguvuni kufikia sasa kimepata kuvutia hisia za viongozi wengi duniani huku sababu za kumfungia msanii huyu zikielezwa kama kutofuata masharti yalikuwepo ya kutofanya fiesta sikukuu iliopita ya pasaka
Kufutilia mbali tamasha zake tatu alizozipanga kunamsababishia hasara kubwa kwa kutumia hela kuyaratibisha. Hali kadhalika inakadamiza haki na uhuru wake wa kutangamana na waganda wenzake
Mwananasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi almaarufu kama Bobi Wine atasalia katika kizuizi cha nyumbani kwa muda usiojulikana.Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa polisi nchini humo. Hatua hii inaaminika wameichukua ili kumzuia mbunge huyu wa Kyadondo Mashariki kutwaa barua rasmi katika makao makuu ya polisi na kuomba ruhusa ya maandamano ya amani .Kwa kufanya kitendo kama hiki kunatishia usalama wa taifa kwa mujibu wa vyanzo mbalimbli nchini humo.
Maswali yasiyo na majibu miongoni mwa wengi ni kwa nini serikali ya Museveni mara kwa mara umzuia mkali huyu kufanya maonyesho pindi tu alipojitosa katika siasa. Waziri wa usalama wa ndani nchini humo ananukuliwa kusema kuwa msanii huyu ukiuka masharti ya kazi anayoekewa.