david.de.gea.ole.gunnar.solskjaer.unai.emery.pierre.emerick.aubameyang.posing.for.the.camera__382095_

Ubashiri A-Z wa mchuano wa Man U na Arsenali, toa maoni yako

Leo mwendo wa saa nne usiku tutashuhudia mchuano mkali katika uwanja wa Old trafford.

Vijana wake Ole Gunnar Solsjaer watakuwa wanawaalika Arsenali.

Ni mechi ambayo imeibua hisia mbali mbali huku kila klabu huenda ikakosa huduma ya wachezaji kadhaa ambao wangetazamiwa kuchangia pakubwa kusaidia klabu yao kushinda.

Nana Owiti asimulia ndoa yake na rapa King Kaka, ataja kukosana

Upande wake mwana Manchester ni kuwa huenda washambulizi wao Marcus Rashford, na Anthony Martial watakosa kucheza mechi hiyo, huku pia kiungo wa kati kutoka Ufaransa Paul Pogba, atakosa kuonyesha makali yake.

Man-Utd-Solskjaer-Pogba-Martial-Rashford-1167179

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solsjaer alianza msimu huu kwa kishindo baada ya kunyuka Chelsea mabao manne kwa bila lakini baada ya mechi sita kuchezwa, ameweza tu kupata pointi nane baada ya kulazwa mabao mawili kwa bila na klabu ya WestHam wiki jana.

Alikiba afichua siri waliyozungumzia na mke wake Amina

Unai Emery ambaye ni mkufunzi wa Arsenal ana matumaini kuwa vijana wake watacheza vizuri hata bila huduma ya mshambuliaji wao Lacazette.

Arsenal ambao walishinda mechi yao dhidi ya Southampton wiki jana, wanatarajia kushinda mechi hiyo.

Unai.Emery.Alexandre.Lacazette.Football365.1

Je, ni nani ataibuka mshindi?

Yote hayo, mwendo wa saa nne usiku.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments