ril

Ubashiri wa ligi ya mabingwa Ulaya

Raundi ya tano ya mabingwa Ulaya itakuwa inachezwa leo usiku huku klabu mbalimbali zikijitahidi kufika katika mkondo utakaofuata baada ya michuano ya vikundi.

Real Madrid vs PSG

Ni mechi kali ambayo mashabiki wengi wa soka wameingoja kwa hamu kwani ni miongoni mwa klabu katika bara Ulaya ambavyo vina uzoefu mkubwa katika ligi hiyo na vile vile wameweza kushinda kombe hilo zaidi ya mara moja.

Makasisi wafungwa miaka 40 kwa kuwanyanyasa watoto

 Katika kundi hilo PSG wanaongoza kwa pointi 12 huku Real Madrid wakiwa na pointi 7 katika nafasi ya pili.

Je, nani mkali? yote hayo yatathibitishwa uwanjani Santiago Bernabue.

Utabiri wangu ni klabu ya PSG itashinda mechi hiyo kwa mabao 3-2.

hazard

Juventus vs Atletico Madrid

Vijana wake Maurizio Sarri watakuwa wanawakaribisha Atletico Madrid nyumbani kwao Allianz. Katika raundi iliyopita Juventus  walitoka sare ya mabao mawili dhidi ya Atletico. Raundi hii itakuaje?

Juventus watakuwa wanategemea sana huduma za Cristiano Ronaldo ambaye alijiunga na klabu hiyo kutoka Real Madrid.

Kwa sasa Juventus wanaongoza katika kundi hilo kwa pointi 10 huku Atletico wakiwa nafasi ya pili na pointi 7.

Utabiri wangu ni klabu ya Juventus itashinda mchuano huo kwa mabao 3-2

roro

Mechi zingine zitakazochezwa leo usiku ni;

Tottenham vs Olympiacos

kane

Manchester City vs Shakhtar Donestsk

silva

 

Crvena vs Bayern Munchen

ndoski

Mwanaume taabani kwa kumwoa mwanafunzi aliyemhadaa kuwa wa miaka 18

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments