Uchaguzi Ganda: Wapiga kura wajitokeza kwa amani baada ya kampeni za fujo

ballot
ballot
Umati mkubwa wa wapiga kura kutoka wadi ya Ganda kaunti ya Kilifi ulijitokeza mapema sana Alhamisi ili kushiriki katika zoezi la kuchagua mwakilishi wao wadi.

Milolongo mirefu imeshuhudiwa katika kituo kikuu cha kuhesabu kura ya shule ya msingi ya Takaye wakiwa na hamu ya kupiga kura. Eneo hilo pia lililo na vituo vitatu vya kupiga kura umeshuhudiwa milolongo mirefu.

Usalama umeimarishwa nje na ndani ya kituo hicho hususana baada ya vurugu vya hivi maajuzi iliyopelekea mtu mmoja kuuawa na hata mwanasiasa Aisha Jumwa kutiwa mbaroni.

Afisa mkuu wa polisi katika kaunti ya Kilifi Patrick Okeri amesema hakuna tukio lolote la ukosefu wa nidhamu ulishuhudiwa katika zoezi hilo,

Hata hivyo Okeri ameonya dhidi ya wale wanaopanga kuvuruga amani waksiema kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.