Handover:Je,Rais Uhuru Kenyatta atampokeza nani kati yao maamlaka 2022?

 7.Moses Wetangula

Kiongozi huyo wa Ford Kenya  na Seneta wa Bungoma hajawahi kuwania urais  lakini wimbo wake umekuwa kwamba lazima atawania kiti hicho mwaka wa 2022 . Iwapo  Wetangula ana ushawishi wa kutosha kupata kora za magharibi katika kapu moja ,ni jambo linalofaa kujadiliwa lakini mambo yalivyo sasa ,itahitaji mambo mengi kubadilisha kwa njia ya haraka sana kumpepeza katika nafasi ya kuweza kabisa kuwatoishia wagombeaji wengine kushinda kiti hicho.Wetang’ula anasalia kuwa katika kundi la viongozi wanaoweza kushinda kiti cha urais baada ya maafikiano ya kabla ya kura ili kuungwa mkono .kama mwanasiasa kivyake ,wakati huu na itakapofika 2022 Wetangula hana uwezo wala hadhi ya kuweza kunyakuwa ushindi  wa kuingia Ikulu bila usaidi mkubwa sana kutoka kwa vigogo wa kisiasa kutoka sehemu mbali mbali za taifa.

8.Wycliffe Oparanya

 Gavana huyo wa Kakamega anayekamilisha muhula wake wa Pili ,amesema kamwe mkondo wake wa siasa ni kuelekea katika siasa za kitaifa .Wadadisi wanasema  Oparanya ana fursa  nzuri sana ya kuweza kuwa rais endapo viongozi wengine wa magharibi watamwunga mkono na kuweka kura zote za magharibi katika kapu moja . Umaarufu wake pia umepigwa jeki na  hatua nzuri  za kimaendelea alizopiga katika kaunti ya Kakamega  katika miaka 7 kama  gavana . Endapo kweli lengo lake ni kuwania na kushinda urais mwaka wa 2022 ,Oparanya kwanza anafaa kuwashawishi wenzake wa magharibi kama vile Eugene Wamalwa ,Musalia Mudavadi na Moses Wetangula kumwunga mkono . Thamani yake kubwa hata hivyo kabla ya chochote kubadilika tunapoelekea uchaguzi  mkuu wa 2022 ,ni kuimarisha tiketi ya mgombea mkuu wa urais  kama mgombea mwenza.