Soma mhabari zaidi;
Harris atapiga jeki kampeni za Biden dhidi ya rais Donald Trump wa Republican huku kukiwa na uhasama wa kijamii kuhusu unyanyasaji wa raia kwa misingi ya rangi na dhulma za polisi dhidi ya wananchi wenye asili ya kiafrika nchini humo.
Biden amekuwa na shinikizo kuchagua mwanamke mwenye asili ya kiafrika kuwa mgombea mwenza wake. Biden na Harris watafanya mkutano wao kwanza pamoja wakiwa kwa tiketi moja ya urais leo Jumatano nyumbani kwake Biden mjini Wilmington, Delaware.
"Ni heshima kubwa sana kumchagua @KamalaHarris — mpiganaji jasiri wa mtu mdogo, na moja wapo wa watumishi bora wa umma - kama mgombea mwenza wangu ," Biden alisema kwa Twitter.
Harris ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kuchaguliwa seneta alipochaguliwa mwaka 2016, atategemewa sana kushawishi kura za watu wenye asili ya kiafrika - ambao wengi wao ni wafuasi wa chama cha Democratic.
Miaka minne iliyopita hatua ya kutopata uungwaji mkono kutoka kwa watu wa asili ya kiafrika kulipelekea mgombeaji wa Democratic Hillary Clinton kubwagwa na Donald Trump.
Soma mhabari zaidi;
Biden ambaye campaign zake za mchujo wa chama cha Democratic ziliokolewa na wapiga kura weusi katika jimbo la South Carolina mwezi Februari, anahitaji sana uungwaji mkono thabiti kutoka kwa wapiga kura weusi dhidi ya Trump. Kivumbi kitatifuliwa katika majimbo kama vile Michigan, Pennsylvania na Wisconsin ambamo Trump alishinda kwa pengo dogo mwaka 2016. Kura za maoni sasa zaonyesha kwamba biden anaongoza katika maeneo hayo.